IQNA

Maonyesho ya  maandishi ya aya za Qur’ani Tukufu katika  kipande cha shaba  huko Karbala

20:49 - May 10, 2026
Habari ID: 3482221
IQNA – Makumbusho ya Al‑Kafeel katika mji wa Karbala yameweka hadharani kipande cha chuma cha shaba kilichochongwa aya za Qur’ani Tukufu kama sehemu ya mkusanyo wake wa turathi.

Makumbusho hayo yako chini ya usimamizi wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS).

Kwa mujibu wa Al‑Kafeel, miongoni mwa vilivyoonyeshwa ni umbo la kiganja cha mkono lililotengenezwa kwa shaba na kuchongwa juu yake aya za Qur’ani, likionyesha pia maana ya ishara na urithi wa sanaa ya uchongaji wa vyuma.

Kipande hicho kina urefu wa sentimita 12 na upana wa sentimita 9.5, kikiwa na uzito wa gramu 103. Aidha kimechongwa tarehe 1221 Hijria, jambo linaloashiria umuhimu wake wa kihistoria na uhusiano wake na kipindi maalumu katika sanaa ya mapambo ya vyuma.

Kipande hiki, chenye umbo la kiganja kilichopambwa kwa michoro ya kijiometri na maandishi ya kisanaa, kimepambwa kwa maneno: “Yadullāh fawqa aydīhim, yā Muhammad, 1221, yā ‘Alī.”

Majina ya Ma’sumina kumi na wanne (AS) pia yamechongwa kwenye vidole na kiganja. Upande mwingine umeandikwa Ayat al‑Kursiy kwenye vidole na kiganja, jambo linaloonesha mchanganyiko wa thamani ya kiroho pamoja na uzuri wa kisanaa.

Kipande hiki kinaonesha umakini na ustadi mkubwa ambao mafundi waliutumia katika sanaa ya uchongaji wa vyuma, pamoja na utofauti wa mitindo ya mapambo iliyotumika.

Kazi hii yenye aya za Qur’ani inachangia kuhifadhi na kuendeleza urithi wa sanaa ya uchongaji wa vyuma kama sehemu muhimu ya utambulisho wa kitamaduni.

3497400

Habari zinazohusiana
captcha